Saturday, July 24, 2010

MARA KWA MARA

Tanzania ni nchi nzuri sana. Watanzania kwa ujumla, pia. Sisi wageni wa muda mdefu tunajua hayo. Uchaguzi unapokuja, tunamwomba Mola amani na utulivu iendelee katika nchi yetu, na katika mioyo wa Watanzania. Leo najiwaza kuhusu uraia mbili na kuhusu green card. Hapa Tanzania sheria ni wazi kabisa na sisi wageni lazima tuiheshimu na tuifuate, sambamba na waraia wenyewe. Kwa hiyo, kila miaka miwili lazima nirudie mkakati wa kuipata hati ya kuishi nchini, na kulipa adha yake. Kwa mfano, dola za merikan 1,600 kama hati yako ni ya daraja la A.

Lakini, mara kwa mara, ningependa wakubwa watufikiries. Kwa sisi tuliokaa muda mdefu katika nchi hii na kwa sababu mbalimbali hatuwezi kupata uraia wa kuomba, hati moja mpya, kama ile Green card ya Ulaya au Merikani ingekuwa nzuri sana. Nchini kwangu, kama mgeni amekaa mfululuzo miaka mitano na ana kazi halali, au ameoa/ameolewa na mraia anapata hati ya kuishi nchini moja pamoja bila tatizo tena. Hapa, kila miaka miwili, lazima siyo tu tulipe adha, ila pia tuanze mpya kila hatua ya mkakati, kuzipeleka documents zote na picha zote tena, na kutumia muda mdefu, na pesa, wakati karibu wageni wote wa muda mdefu hapa tunakuwa watu wa kupenda maendeleo ya nchi kwa sababu maendeleo ya nchi ni maendeleo yetu.
Sijui. Pengine baada ya Uchaguzi na katika kuiongelea sheria ya uraia mbili hapo mbele, wabunge wanaweza pia kufikiri namna ya kuweza kuwasaidia wale tuliokaa muda mdefu hapa, tunalipa kodi zetu, tunashirikiana kwa kuijenga nchi na tunapenda nchi yetu. Mungu ibariki Tanzania.

No comments:

Post a Comment